Airtel

Airtel
Twanga kotekote

Tuesday, January 19, 2021

DIAMOND ALIVYOJIBU SUALA LA BABA YAKE..!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Media Naseeb Abdul, maarufu kwa jina la Diamond Platinumz amekataa kuzungumzia habari ambazo zimekuwa zikizungumzwa kwenye mitandao mbalimbali jamii zinazoihusu familia yake.

Akijibu swali la mmoja wa Waandishi wa habari jijini Dar es salaam aliyetaka kujua majina yake halisi atakayokuwa anayatumia kwa sasa, Diamond amesema suala hilo atalizungumzia siku nyingine.

“Masuala ya chumbani hayapaswi kuwekwa hadharani, hivyo suala hili nitalizumgumzia siku nyingine ila kwa sasa tuzungumze juu ya tamasha lililoko mbele yetu kwa ajili ya Watanzania,” amesema Diamond.

Aidha, Diamond amewataka Watanzania kuyapa kipaumbele mambo yenye maslahi kwa Taifa badala ya kukaaa mitandaoni kufuatilia vitu ambavyo havina tija kwa Taifa.

Kauli ya Msanii huyo imekuja zikiwa zimepita siku chache baada ha kuibuka kwa sintofahamu juu ya baba halisi wa Msanii huyo.

Saa za Trump White House zayoyoma

 


Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani, Joe Biden zinatarajiwa kufanyika kesho majira ya mchana kwa saa za Marekani.

Mwanamuziki Lady Gaga  anatarajiwa kuimba wimbo wa Taifa hilo katika hafla hiyo  ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wachache.

Makamu wa Rais Kamala Harris ataapishwa kabla ya Biden  kuapishwa na kuhutubia.

Ulinzi umeimarishwa maradufu katika jiji la Washington DC ambapo maelfu ya askari wameongezwa katika jiji hilo.

Rais Mteule Biden  na Makamu wa Rais mteule Kamala  wanatarajiwa kuwasili jijini Washington  hii leo kwa ndege.

Aidha baadae leo ibada maalum inatarajiwa kufanyika kuwakumbuka maelfu ya watu waliofariki duniani  baada ya kuugua Corona nchini Marekani.

Monday, January 18, 2021

MADARASA YAMEBOMOKA, MKUU WA MKOA YUPO NA MKURUGENZI ANAKUSANYA KODI - RAIS MAGUFURI

Rais John Pombe Magufuri amesikitishwa na kitendo cha Viongozi wa Mkoa wa Dsm kutoshughulikia masuala ya elimu na kuacha wanafunzi kuendelea kukaa chini na kusoma kwenye majengo mabovu. 


”Kuna shule moja ya msingi Ubungo Dar Es Salaam inatwa Barango, ina wanafunzi wengi tu. Shule hiyo wanafunzi wapo Dar Es Salaam Ubungo bado wana kaa chini, madarasa mengine yamebomoka, madawati mengine yamevunjika yameachwa bure, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena yupo hapa na ni profesa tena wa Elimu, simama profesa wakuone kwenye jimbo lako, anafundisha elimu, mimi napenda kusema uwazi.” Rais Magufuli akifungua majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Kagera

”Lakini hiyo shule ya Ubungo Barango wanakaa chini, nina mshukuru huyo mwandishi ameitoa kwenye mitandao, viongozi wa kule wakaanza kusema ni maswala ya kisiasa, hayo sio maswala ya kisiasa hayo ndiyo ninayopenda kuyajua. Ninazungumza nikiwa Kagera lakini nikienda Dar Es Salaam niyakute hayo madarasa yamekamilika na wanafunzi hawakai chini, nitaenda kuitembelea hiyo shule kama wananisikia wa Dar Es Salaam ujumbe umefika.” Rais Magufuli akifungua majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Kagera

Thursday, January 14, 2021

TMA Yatoa Tahadhari ya MVUA Kubwa Kesho



TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa itakayonyesha kesho Ijumaa Januari 15, 2021 husu siku zinazofuata zikitarajiwa kuwa shwari hadi Januari 18.


Dar es Salaam . Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa itakayonyesha kesho Ijumaa Januari 15, 2021 huku siku zinazofuata zikitarajiwa kuwa shwari hadi Januari 18.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Alhamisi Januari 14, 2021 inaeleza kuwa utabiri huo wa siku tano kuanzia leo unaonyesha mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini.


Tahadhari hiyo ya mvua kubwa imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tabora, Singida, Dodoma, Ruvuma, Mahenge, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe huku uwezekano wa kutokea kwa utabiri huo ukiwa wa wastani.


“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji,” inaeleza taarifa hiyo ya TMA.

Wednesday, August 7, 2019

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI MKE WA MWANASHERIA MKUU



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 7, 2019 ameiwakilisha serikali katika mazishi ya Natalia Baraka Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi. Mazishi hayo yamefanyika eneo la Luchelele jijini Mwanza. 

Monday, July 29, 2019

PAUL MAKONDA: WASIOFUA NGUO, KUNYOOSHA, KUOGA MARUFUKU DSM HADI MKUTANO WA SADC UMALIZIKE



Mkuu wa Mkoa wa Dar amepiga marufuku watu wachafu kuonekana maeneo ya katikati ya mji hasa wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

Makonda amesema kuja mjini bila kunyoosha nguo na kuoga ni marufuku. Wapo wanaotembea na chawa. Kama huwezi kuwa msafi basi subiri mkutano upite

Amesisitiza kuwa hataki kumtia aibu Rais Magufuli mbele ya Marais kutoka nchi 15 watakaokuwa hapa nchini

Ameyasema hayo leo wakati akizindua kampeni ya usafi ikiwa ni moja ya maandalizi ya mkutano wa 39 wa SADC unaotarajiwa kufanyika hapa nchini Agosti 17 na 18, 2019.

Waziri LUGOLA amtumbua RTO ARUSHA kutotii maagizo



Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuondoa madarakani Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa madai ya kupuuza maagizo yake na kuyaita ya kisiasa

Taarifa ya Wizara hiyo imeeleza kuwa Waziri Lugola amemuagiza pia Katibu Mkuu wa wizara, kumchukulia hatua za kinidhamu Askari huyo ili iwe fundisho kwa wengine

Lugola amesema amemshuhudia Bukombe katika video inayosambaa mitandaoni alipokuwa katika mkutano jijini Arusha akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na hakuyatekeleza


Aidha, akiwa katika mkutano wa hadhara katika mji wa Malinyi mkoani Morogoro jana, Lugola amesema hatoi maagizo ya kisiasa ila hutoa yanayomsaidia Rais Magufuli

Friday, July 26, 2019

Rais MAGUFULI aiagiza Wizara ya Fedha kifanya Uchunguzi, ni kuhusu Mabilioni ya TAZARA


Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuchunguza matumizi ya Tsh Bilioni 15 na Milioni 300 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia matumizi ya TAZARA 

John Bocco ateuliwa NAHODHA timu ya Taifa


Kaimu Kocha Mkuu taifa stars, Ndayiragije Etienne amemteua mshambuliaji John Bocco kuwa nahodha wa timu ya Taifa kwa wachezaji wa ndani akisaidiwa na Juma Kaseja, Erasto Nyoni na Kelvin Yondan

Stars inajiandaa na mchezo wa CHAN dhidi ya Kenya jumapili July 28 uwanja wa Taifa. 

Thursday, July 25, 2019

TANZANIA KUIUZIA KENYA MAHINDI


Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali itaiuzia Kenya Mahindi tani milioni 1 katika kipindi cha mwaka 1, baada ya msimu wa mvua kugoma nchini humo hali inayotishia kuwepo kwa upungufu wa chakula

Amesema kuwa wamekubaliana kwa wiki ijayo watakutana na kufanya kikao kitakachozikutanisha idara zote za mapato na masuala ya viwango na ubora wa bidhaa kutoka nchi ya Kenya na Tanzania pamoja na sekta zote zinazohusika na mauzo ya chakula

Aidha, hatua hiyo imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kenya, Profesa Fred Segor, kusema mwaka huu wana changamoto ya hali ya hewa, kwa kuwa mvua haikunyesha ipasavyo

DC SABAYA KUCHUNGUZWA KUHUSU TUHUMA ZA RUSHWA, MWENYEWE AKANUSHA VIKALI



Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, anachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutokana na malalamiko yaliyotolewa, kwamba analazimisha wafanyabiashara kumpa rushwa

Mfanyabiashara wa utalii wa Kampuni ya Asante Tours, Cathberty Swai, alimtuhumu Sabaya kumpa vitisho na kudai fedha kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kuwakamata wafanyakazi wake na kuwaweka mahabusu

Swai alisema hayo katika kikao cha wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania kilichofanyika jana Moshi mkoani Kilimanjaro

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu amesema ofisi yake ipo katika mchakato wa kuzungumza na mfanyabiashara huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa

Swai alidai Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa ni kikwazo kwa wawekezaji na licha ya kulipa kodi Serikalini, kiasi cha Tsh. milioni 148 kwa mwaka, lakini amekuwa akipokea vitisho na manyanyaso kutoka kwa Sabaya na kumlazimisha kumpa fedha

Hata hivyo, Sabaya alikana tuhuma hizo na kutangaza kumnyang’anya mfanyabiashara huyo mashamba yake, na kuagiza polisi kumkamata

SIEMENS KUBORESHA UMEME NIGERIA



Serikali ya Nigeria imeingia makubaliano hayo ili kuhakikisha nchi inapata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2025

Mtendaji Mkuu wa Siemens, Joe Kaeser amemuahidi Rais Buhari kuwa miundombinu itakayojengwa na kampuni hiyo itazalisha Megawati 25,000 za umeme ifikapo mwaka 2025

Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari asema nishati ya umeme ni msingi wa maendeleo ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla

Wednesday, July 24, 2019

Rais MAGUFULI Apokea KG 35.34 za Dhahabu kutoka Kenya



Dhahabu hii ilikamatwa Februari 15, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta wakati Baraka Chaulo akiisafirisha kupitia Ndege ya Shirika la Precision Air

Aidha, tukio hili linahusisha pia makabidhiano ya fedha zilizoibwa NBC Tawi la Moshi mwaka 2004 zilizokamatwa nchini Kenya

Fedha hizo (Tsh. Milioni 170, Dola za Marekani 76,500 na Shilingi za Kenya 171,600) kama sehemu ya ushahidi zilikuwa zimehifadhiwa Kenya kwa wakati wote huo.