Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, anachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutokana na malalamiko yaliyotolewa, kwamba analazimisha wafanyabiashara kumpa rushwa
Mfanyabiashara wa utalii wa Kampuni ya Asante Tours, Cathberty Swai, alimtuhumu Sabaya kumpa vitisho na kudai fedha kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kuwakamata wafanyakazi wake na kuwaweka mahabusu
Swai alisema hayo katika kikao cha wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania kilichofanyika jana Moshi mkoani Kilimanjaro
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu amesema ofisi yake ipo katika mchakato wa kuzungumza na mfanyabiashara huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
Swai alidai Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa ni kikwazo kwa wawekezaji na licha ya kulipa kodi Serikalini, kiasi cha Tsh. milioni 148 kwa mwaka, lakini amekuwa akipokea vitisho na manyanyaso kutoka kwa Sabaya na kumlazimisha kumpa fedha
Hata hivyo, Sabaya alikana tuhuma hizo na kutangaza kumnyang’anya mfanyabiashara huyo mashamba yake, na kuagiza polisi kumkamata

No comments:
Post a Comment