Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuondoa madarakani Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa madai ya kupuuza maagizo yake na kuyaita ya kisiasa
Taarifa ya Wizara hiyo imeeleza kuwa Waziri Lugola amemuagiza pia Katibu Mkuu wa wizara, kumchukulia hatua za kinidhamu Askari huyo ili iwe fundisho kwa wengine
Lugola amesema amemshuhudia Bukombe katika video inayosambaa mitandaoni alipokuwa katika mkutano jijini Arusha akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na hakuyatekeleza
Aidha, akiwa katika mkutano wa hadhara katika mji wa Malinyi mkoani Morogoro jana, Lugola amesema hatoi maagizo ya kisiasa ila hutoa yanayomsaidia Rais Magufuli

No comments:
Post a Comment