Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuchunguza matumizi ya Tsh Bilioni 15 na Milioni 300 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia matumizi ya TAZARA
Airtel
Twanga kotekote
Friday, July 26, 2019
Thursday, July 25, 2019
TANZANIA KUIUZIA KENYA MAHINDI
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali itaiuzia Kenya Mahindi tani milioni 1 katika kipindi cha mwaka 1, baada ya msimu wa mvua kugoma nchini humo hali inayotishia kuwepo kwa upungufu wa chakula
Amesema kuwa wamekubaliana kwa wiki ijayo watakutana na kufanya kikao kitakachozikutanisha idara zote za mapato na masuala ya viwango na ubora wa bidhaa kutoka nchi ya Kenya na Tanzania pamoja na sekta zote zinazohusika na mauzo ya chakula
Aidha, hatua hiyo imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kenya, Profesa Fred Segor, kusema mwaka huu wana changamoto ya hali ya hewa, kwa kuwa mvua haikunyesha ipasavyo
DC SABAYA KUCHUNGUZWA KUHUSU TUHUMA ZA RUSHWA, MWENYEWE AKANUSHA VIKALI
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, anachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutokana na malalamiko yaliyotolewa, kwamba analazimisha wafanyabiashara kumpa rushwa
Mfanyabiashara wa utalii wa Kampuni ya Asante Tours, Cathberty Swai, alimtuhumu Sabaya kumpa vitisho na kudai fedha kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kuwakamata wafanyakazi wake na kuwaweka mahabusu
Swai alisema hayo katika kikao cha wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania kilichofanyika jana Moshi mkoani Kilimanjaro
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu amesema ofisi yake ipo katika mchakato wa kuzungumza na mfanyabiashara huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
Swai alidai Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa ni kikwazo kwa wawekezaji na licha ya kulipa kodi Serikalini, kiasi cha Tsh. milioni 148 kwa mwaka, lakini amekuwa akipokea vitisho na manyanyaso kutoka kwa Sabaya na kumlazimisha kumpa fedha
Hata hivyo, Sabaya alikana tuhuma hizo na kutangaza kumnyang’anya mfanyabiashara huyo mashamba yake, na kuagiza polisi kumkamata
SIEMENS KUBORESHA UMEME NIGERIA
Serikali ya Nigeria imeingia makubaliano hayo ili kuhakikisha nchi inapata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2025
Mtendaji Mkuu wa Siemens, Joe Kaeser amemuahidi Rais Buhari kuwa miundombinu itakayojengwa na kampuni hiyo itazalisha Megawati 25,000 za umeme ifikapo mwaka 2025
Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari asema nishati ya umeme ni msingi wa maendeleo ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla
Wednesday, July 24, 2019
Rais MAGUFULI Apokea KG 35.34 za Dhahabu kutoka Kenya
Dhahabu hii ilikamatwa Februari 15, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta wakati Baraka Chaulo akiisafirisha kupitia Ndege ya Shirika la Precision Air
Aidha, tukio hili linahusisha pia makabidhiano ya fedha zilizoibwa NBC Tawi la Moshi mwaka 2004 zilizokamatwa nchini Kenya
Fedha hizo (Tsh. Milioni 170, Dola za Marekani 76,500 na Shilingi za Kenya 171,600) kama sehemu ya ushahidi zilikuwa zimehifadhiwa Kenya kwa wakati wote huo.
IMF: UCHUMI WA DUNIA WAZIDI KUDORORA
Ripoti mpya ya robo mwaka kuhusu uchumi wa dunia ya shirika la Fedha Duniani, imeonesha ukuaji mdogo wa uchumi kidunia huku ikionya kuhusu vita vya kibiashara, uwezekano wa kukosekana kwa mkataba wa Brexit na changamoto nyingine zinazochangia kudorora kwa uchumi
Ripoti hiyo inasema kuwa mizozo ya kibiashara imepunguza kasi ya uwekezaji na kudorora kwa sekta ya viwanda na imetoa wito kwa mataifa kutotumia tozo kumaliza tofauti zao
Uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa kasi ndogo ambapo katika mwaka 2019 uchumi wa unatarajiwa utakuwa kwa asilimia 3.2 na asilimia 3.5 kwa mwaka 2020
Aidha, shirika hilo limesema ikiwa hali ya sasa itaendelea kushuhudiwa mfululizo, basi huenda mambo yakawa mabaya zaidi kwa mataifa mengi na hasa yale yanayoendelea
Tuesday, July 23, 2019
Uzinduzi Kituo cha Mabasi, Rc Hapi atema CHECHE
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ally Hapi akitoa hotuba mara baada ya kufanya uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Mkoa wa Iringa kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Hapi amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Hamid Njovu kuvuta umiliki wa viwanja vyote vinavyozunguka Kituo hicho cha Mabasi Igumbilo mpaka pale Utaratibu mpya utakapofanyika.
Subscribe to:
Comments (Atom)








