Airtel

Airtel
Twanga kotekote

Tuesday, January 19, 2021

DIAMOND ALIVYOJIBU SUALA LA BABA YAKE..!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Media Naseeb Abdul, maarufu kwa jina la Diamond Platinumz amekataa kuzungumzia habari ambazo zimekuwa zikizungumzwa kwenye mitandao mbalimbali jamii zinazoihusu familia yake.

Akijibu swali la mmoja wa Waandishi wa habari jijini Dar es salaam aliyetaka kujua majina yake halisi atakayokuwa anayatumia kwa sasa, Diamond amesema suala hilo atalizungumzia siku nyingine.

“Masuala ya chumbani hayapaswi kuwekwa hadharani, hivyo suala hili nitalizumgumzia siku nyingine ila kwa sasa tuzungumze juu ya tamasha lililoko mbele yetu kwa ajili ya Watanzania,” amesema Diamond.

Aidha, Diamond amewataka Watanzania kuyapa kipaumbele mambo yenye maslahi kwa Taifa badala ya kukaaa mitandaoni kufuatilia vitu ambavyo havina tija kwa Taifa.

Kauli ya Msanii huyo imekuja zikiwa zimepita siku chache baada ha kuibuka kwa sintofahamu juu ya baba halisi wa Msanii huyo.

Saa za Trump White House zayoyoma

 


Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani, Joe Biden zinatarajiwa kufanyika kesho majira ya mchana kwa saa za Marekani.

Mwanamuziki Lady Gaga  anatarajiwa kuimba wimbo wa Taifa hilo katika hafla hiyo  ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wachache.

Makamu wa Rais Kamala Harris ataapishwa kabla ya Biden  kuapishwa na kuhutubia.

Ulinzi umeimarishwa maradufu katika jiji la Washington DC ambapo maelfu ya askari wameongezwa katika jiji hilo.

Rais Mteule Biden  na Makamu wa Rais mteule Kamala  wanatarajiwa kuwasili jijini Washington  hii leo kwa ndege.

Aidha baadae leo ibada maalum inatarajiwa kufanyika kuwakumbuka maelfu ya watu waliofariki duniani  baada ya kuugua Corona nchini Marekani.

Monday, January 18, 2021

MADARASA YAMEBOMOKA, MKUU WA MKOA YUPO NA MKURUGENZI ANAKUSANYA KODI - RAIS MAGUFURI

Rais John Pombe Magufuri amesikitishwa na kitendo cha Viongozi wa Mkoa wa Dsm kutoshughulikia masuala ya elimu na kuacha wanafunzi kuendelea kukaa chini na kusoma kwenye majengo mabovu. 


”Kuna shule moja ya msingi Ubungo Dar Es Salaam inatwa Barango, ina wanafunzi wengi tu. Shule hiyo wanafunzi wapo Dar Es Salaam Ubungo bado wana kaa chini, madarasa mengine yamebomoka, madawati mengine yamevunjika yameachwa bure, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena yupo hapa na ni profesa tena wa Elimu, simama profesa wakuone kwenye jimbo lako, anafundisha elimu, mimi napenda kusema uwazi.” Rais Magufuli akifungua majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Kagera

”Lakini hiyo shule ya Ubungo Barango wanakaa chini, nina mshukuru huyo mwandishi ameitoa kwenye mitandao, viongozi wa kule wakaanza kusema ni maswala ya kisiasa, hayo sio maswala ya kisiasa hayo ndiyo ninayopenda kuyajua. Ninazungumza nikiwa Kagera lakini nikienda Dar Es Salaam niyakute hayo madarasa yamekamilika na wanafunzi hawakai chini, nitaenda kuitembelea hiyo shule kama wananisikia wa Dar Es Salaam ujumbe umefika.” Rais Magufuli akifungua majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Kagera

Thursday, January 14, 2021

TMA Yatoa Tahadhari ya MVUA Kubwa Kesho



TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa itakayonyesha kesho Ijumaa Januari 15, 2021 husu siku zinazofuata zikitarajiwa kuwa shwari hadi Januari 18.


Dar es Salaam . Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa itakayonyesha kesho Ijumaa Januari 15, 2021 huku siku zinazofuata zikitarajiwa kuwa shwari hadi Januari 18.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Alhamisi Januari 14, 2021 inaeleza kuwa utabiri huo wa siku tano kuanzia leo unaonyesha mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini.


Tahadhari hiyo ya mvua kubwa imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tabora, Singida, Dodoma, Ruvuma, Mahenge, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe huku uwezekano wa kutokea kwa utabiri huo ukiwa wa wastani.


“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji,” inaeleza taarifa hiyo ya TMA.